WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Wednesday 13 July 2016

UMUHIMU WA KUJENGEA UWEZO WATU WETU KATIKA KUBABILIANA NA UHALIFU MTANDAO

Uhalifu mtandao bado umeendelea kukua maeneo mbali mbali Duniani – Tishio hili linachukua sura ya kipekee wakati ambapo uhalifu mtandao ume endelea kufanyika kwa ustadi wa hali ya juu huku ukindelea kukua kwa kasi ya kipekee.

Ujuzi mkubwa walionao wahalifu mtandao unatosha kua somo kwa wanaopambana na uhalifu mtandao kujipanga zaidi hasa ukizingatia namna ya ufanyai uhalifu mtandao, umeendelea kubadilika kadri teknolojia inavyobadilika sanjari na inavyokua.

Kuzingatia yote haya moja ya maazimio tuliokubaliana Jijini Johannesburg, Afrika kusini mwaka jana (2015) ni kuhakiki ya kua situ tunakua na watu sahihi wenye ujuzi wa kupambana na uhalifu mtandao bali pia kujenga tabia ya kuwaongezea uwezo na kutengeneza nguvu kazi zetu zitakazo saidia mapambano dhidi ya Uhalifu Mtandao Barani na Duniani kwa ujumla.

Nchi mbalimbali barani zimeendelea kulifanyia kazi hili ikiwa ni pamoja na kupitia upya mitaala yake ili kuhakiki elimu sahihi ya maswala ya usalama mitandao inafundishwa na kuhimiza tabia ya wahusika kuendelea kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara pamoja na kujijengea tabia ya kujifunza kwa kupitia yale yanayo andikwa na wataalam wa usalama mtandao ili kufahamu kinachoendelea katika fani husika kwani Mbinu za kihalifu mtandao zimekua zikibadilika sana kadri teknolojia inavyo badilika pamoja na kukua.

Binafsi, Nilipokea mwaliko katika Kauti ya Bungoma Nchini Kenya ili kushuhudia na kushauri mpango mpya wa kauti hiyo wa kuanzisha maabara maalum zilizo dhamiriwa kua ni za kutengeneza wataalam wa usalama mitandao watakao saidia kukabiliana na uhalifu mtandao si katika kauti pekee bali ni pamoja na Nchi nzima ya Kenya.


----------------------------------------
NEWS UPDATES: A new free online tool for the notification of personal data breaches has been developed by ENISA, in co-operation with the Office of the Federal Commissioner for Data Protection and Freedom of Information of Germany (German DPA).
The purpose of the tool is to allow data controllers to complete and submit online a personal data breach notification to the competent authority.
----------------------------------------

Nilikubali mwaliko huo, na nilipo zuru Kauti hiyo nilipata kushiriki mambo kadhaa. Kubwa ikiwa ni kutembeea Mradi huo wa uanzishwaji wa Maabara maalum ya kutengeneza na kukuza vipaji katika fani ya usalama mtandao sanjari na kuzungumza na wanafunzi wanaodhaminiwa na serikali ya Nchi ya Kenya ili kuweza kutengeneza mifumo mbali mbali itakayoweza kutumika katika simu.

Katika mazungumzo yangu na Vijana hao nili wahimiza kuwa natabia ya kujisomea mara kwa mara maswla ya usalama mtandao ili kujua yanayojiri na suluhu mbali mbali zinazoendelea kupatikana kutoka kwa wataalam wa uslama mitandao wanaopatikana maeneo yote duniani.

Aidha, Niliwataka wasiwe tu wanajifunza ili kuweza kujua na kuwa wataalam tu wa maswala ya usalama mtandao bali wajue wanatakiwa kuwa na uzalendo wa dhati na kujua wanadhamana kubwa ya kuhakiki wanakabiliana ipasavyo na uhalifu mtandao ili baadae na wao wasijikute wametumbukia katika vitendo vya kihalifu mtandao.

---------------------------------------
NEWS UPDATES: Fast-food chain Wendy's says a cyberattack that stole payment card details affected 1,025 U.S. restaurants owned by franchisees, a far higher figure than first estimated.
-------------------------------------------

Shughuli nyingine nilizo pata kushiriki ni pamoja na kushiriki mahafali ya wahitimu wa chuo kimoja katika kauti hiyo sanjari na kuzuru Chuo kikuu cha Kibabii ambapo pia nilipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi wa Shahada ya Uzamili wa maswala ya TEHAMA.

Katika mazungumzo yangu na wanafunzi hao  niliwahamasisha kujenga tabia ya kujifunza fani hii ya usalama mtandao kwani kwa sasa imeendelea kua muhimu sana maeneo mengi sanjari na kuwahimiza waifunzapo maswala ya usalama mtandao wajitahidi kuwa katika upande wa kuzuia na wasije kua ni changamoto kwa kupelekea ukuaji wa Uhaliffu mtandao.

Nichukue fursa hii kupongeza juhudi za serikali ya Kauti ya Bungoma ya nchi ya Kenya kwa kuanzisha mpango huo muhimu ambao naimani kubwa utakua na Manufaa makubwa hasa kipindi hiki ambacho wahalifu mtandao wameendelea kua na mbinu mpya madhubuti za kutekeleza uhalifu mtandao na nimategemeo yangu zao la jitihada hizi litakua chanya na kua msaada mkubwa kwa taifa hilo la Nchi ya Kenya katika upambanaji na uhalifu mtandao.


Aidha, nitoe wito kwa mataifa mengine hususan mataifa ya jumuia ya Afrika mashariki kujua wana dhamana ya kuhakiki rasilimali za jumuia ya Afrika mashhariki zinaendelea kulindwa ipasavyo dhidi ya wahaifu mtandao  – Hivyo pawe na dhamira ya dhati za kuhakiki tunaendelea kutengeneza watu wetu katika fani hii ambao watakua ni msaada kwetu katika kukabiliana na uhalifu mtandao.


No comments:

Post a Comment