WELCOME !

THANK YOU FOR VISITING THIS SITE. I HAVE BEEN USING BOTH SWAHILI AND ENGLISH LANGUAGE TO EXPRESS ISSUES - I HAVE ATTACHED ENGLISH VERSION TO SOME OF THE SWAHILI NEWS/STORY AT THE END.

Saturday 28 April 2018

KENYA: WAKUU WA TEHAMA WAKUTANA



KWA UFUPI: Wakuu wa vitengo vya TEHAMA wamekutana kujadili changamoto na namna nzuri ya kuzitatua changamoto hizo katika vikao vilivyo kamilika Nchini Kenya.
-------------------------------

Watunga sera na sheria mbali mbali wamekua wakifanya maamuzi ya TEHAMA bila kushirikisha wadau wa TEHAMA – Hii imekua moja ya changamoto inayo leta mkinzano wa utendaji wenye manufaa kwa wana TEHAMA maeneo mengi barani Afrika.

Mjadala ulioangazia umuhimu wa udhibiti na uangalizi wa watendaji katika sekta ya TEHAMA umeonekana kua mzuri ila umegubikwa na changamoto kadhaa kutokana na ushirikishwaji mdogo wa wadau ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye sekta husika.

Mjadala huu umejadiliwa kufuatia kuwepo kwa sera mpya nchini Kenya itakayo rasimisha Wana TEHAMA na kuwataka watambulike kabla ya kuweza kuhudumu maeneo mbali mbali. Hili litafanana na tulicho nacho nchini Tanzania kwa wanasheria pamoja na wataalam wa maeneo mengine kadhaa.


Kinachotegemewa katika urasimishaji wa sekta ya TEHAMA na kumfanya mwana TEHAMA atambulike na kuhudumia katika sekta ya TEHAMA ni pamoja na  kupitia hatua kuu tatu ambazo ni, Kusomea – Usaili – Kupatiwa leseni ya kutoa huduma katika sekta husika.

Changamoto iliyo onekana ni pamoja na uwezekano wa kuua vipaji vya wabunifu wa TEHAMA ambao wamekua wakija na ubunifu wenye manufaa pasi na kua na ujuzi rasmi katika sekta husika.

Tumeshudia kuwepo kwa vijana walio somea fani nyingine tofauti na TEHAMA ila baadae kuja na Mifumo mizuri ya Kitehama iliyoweza kutatua changamoto mbali mbali katika maeneo yetu tofauti na wengine waliosomea fani husika na kushindwa kuwa wabunifu wa kuleta mabadiliko katika jamii zetu.

Kuna baadhi ya Mifumo tuko nayo maeneo mengi ambayo wabunifu wake hawakua na elimu ramsi katika sekta ya TEHAMA. Aidha, Swali kuu matumizi ya TEHAMA ya mekua kuna ulazima mhusika kua na elimu rasmi? Ilhali kila sekta inategemea TEHAMA na kuna uwezekano kila mwenye ujuzi wa fani yoyote akawa na uwezo wa kufanya vizuri kwenye mifumo ya TEHAMA.



GDPR (General Data Protection Regulations) Nchi za umoja wa ulaya wana mategemeo ya kuanza rasmi matumizi ya GDPR mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu wa 2018 – Lengo kuu ni kulinda faragha za raia wake.

Hatua hii inaweza kuathiri maeneo mengi duniani Afrika ikiwemo kwani tumeendelea kufanya biashara na kuhudumia mataifa ya umoja wa ulaya ambapo inahusisha taarifa za wana jumuia ya ulaya kupatikana kwetu.

Mjadala mzito wa nini tutegemee pale umoja wa Ulaya watakapo anza rasmi matumizi ya GDPR katika taasisi zetu hususan za kifedha. Namna bora ya kuweza kulinda (faragha) za watumiaji mifumo ya kitehama katika taasisi zetu ili kuondokana na tunachoweza kukabiliana nacho baada ya kuanza rasmi matumizi ya GDPR barani ulaya.



CSIRT (Computer Security Incidence Response Team) – Tumekua na changamoto ya uwepo wa vitengo mahususi vya kukabiliana na matukio ya kihalifu mtandao katika taasisi na kampuni mbali mbali. Hili linatokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa vitengo hivi mahsusi vyenye jukumu la kukabiliana na uhalifu mtandao.

Umuhimu wa CSIRT, namna ya kuanzisha na majukumu yake katika kila kampuni na taasisi ni mjadala nilio uongoza kuhakiki kila mmoja anafahamu hili.

Matukio ya kihalifu mtandao katika mataifa yetu yanayopelekea upotevu wa Fedha, upotevu wa taarifa, udukuzi wa mifumo na kadhalika yamekua yakijitokeza mara kwa mara yanayo acha athari kubwa kwa taasisi za serikali na binafsi maeneo mengi duniani.

Ni wajibu wa kila taasisi na kampuni kujua ina jukumu la kujilinda dhidi ya uhalifu mtandao na namna pekee ya kufikia hapo ni pamoja na kua na kitengo wahususi chenye jukumu la ulinzi mtandao pekee ambapo kitengo husika kitaweza kuhakiki usalama mtandao unakuwepo.


Aidha, kumekua na mijadala mingine mingi sana ambayo yote ilikua na lengo la kuhakiki tuna tambua namna sahihi ya kukabiliana na changamoto nyingi zinazotokana na uwepo matumizi makubwa ya mifumo ya TEHAMA yanayo rahisisha utendaji kazi katika taasisi na kampuni mbali mbali.

14 comments: